Isaya 11

Ufalme wa Amani πŸ•― Sura ya 10 iliishia kwa Bwana kuzungumzia namna ambavyo angeshughulika na Waashuru na kuwaadhibu kwa kiburi chao. Lakini Bwana hawaachi wana masalia wake bila tumaini. Wakati Bwana angekata vichaka vya Ashuru kwa chuma kwa Israeli hali ikikiwa tofauti. Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake…

Isaya 10

⚠️ Fungu la 1 – 4 ni mwendelezo wa sura ya 9 ambapo Bwana anazungumzia kutoridhishwa kwake na udhalimu wa watawala kupora haki za wanyonge, wajane na yatima. Bwana anaonesha dhahiri kutoridhishwa na hali hiyo na ya kwamba iko siku angechukua hatua na hakuna mkono ambao ungewaokoa na ghadhabu yake. Kiburi cha Ashuru ⚠️ Kama…

Isaya 8

πŸ”Š Kama kuna kitu kikubwa tunajifunza ni namna Isaya na familia yake kwa ujumla walitumiwa na Bwana kuwa ujumbe ulio hai. πŸ”Š Bwana alimwambia nabii kuandika neno Maher-shalal-hash-bazi; lakini kama haikutosha nabii alipopata mtoto pia alimpa jina jina hilo lenye maana ‘yenye wepesi wa kuharibu na kuteka.’ Neno la Bwana likasema kabla mtoto huyo hajaweza…

Isaya 7

Ahadi ya Ukombozi πŸ•― Katika kipindi cha mjukuu wa mfalme Uzia mfalme Ahazi, mfalme alikabiliwa na tishio la kuangamizwa na ushirikiano wa falme za Kaskazini (Efraimu) na Shamu. Mataifa hayo yaliiomba Yuda kuungana nayo kuishambulia Ashuru lakini Ahazi alikataa kwa kuwa alikuwa ameingia makubaliano ya ushirikiano ya siri na Ashuru, hivyo mataifa hayo yakakusudia kumng’oa,…

Isaya 6

Utume wa Isaya Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. β™Ÿ Utawala wa mfalme Uzia ulikuwa wenye ustawi na taifa lilimpenda sana, hivyo kifo chake kiliacha taifa katika huzuni kubwa lakini hofu yao zaidi ilikuwa ni…

Isaya 4

Chipukizi la Bwana Latukuzwa Katika siku ile wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, β€œTutakula chakula chetu wenyewe na kuvaa nguo zetu wenyewe, ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako. Utuondolee aibu yetu!” β™Ÿ Fungu hili ni mwendelezo wa kisa katika sura ya 4 ambapo adhabu ya Bwana katika Israeli itaacha Yuda bila mashujaa wake,…

Isaya 2

Katika siku za mwisho mlima wa hekalu la BWANA utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima, utainuliwa juu kupita vilima na mataifa yote yatamiminika huko. ✍🏾 Kinyume na matendo ya Waisraeli ya kwenda huku na huko kutafuta miungu mingine ya kuabudu, wakati wa mwisho mataifa yote yatamiminika Israeli kwenda kumtafura Bwana wa Yakobo. Wataenda katika…

Isaya 1

Uovu wa Yuda Utangulizi Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi, aliyoyaona katika habari za Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia na Yothamu na Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. Kama ambavyo tumeona wakati wote muda hapo kale ulipimwa kwa kurejea mtawala aliyekuwa madarakani ikitaja mwaka wake wa utawala. Isaya alifanya huduma yake katika…

Wimbo Ulio Bora 6

Kuachilia 🀝 Baada ya kuhitimisha kwa kuwaelezea marafiki kuwa alikuwa akimtafuta mpenzi wake, marafiki zake wanasikika kumuulizia maendeleo yake na kutaka kufahamu endapo alishampata au waendelee kumsaidia kumtafuta. 🀝 Lakini awamu hii malkia alikuwa na habari njema kwa rafiki zake: Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma…

Wimbo Ulio Bora 2

Uchumba – 2 Mimi ni ua la uwandani, ni nyinyoro ya mabondeni. πŸ‘« Mashaka. Kauli hii ya binti wa Shunami ilikuwa ya mashaka na kuhisi kupungua kama ua lililoota uwandani pasipo na huduma nzuri au nyiroro ya mabondeni. Mara nyingi mabinti wachumbiwapo na watu wanaowaona kuwa wenye hadhi kuwazidi hujawa na mashaka, haya na hofu…